Upendo SACCOS

Image

Kikundi cha Akiba na Mikopo "Upendo Saccos LTD" kilianzishwa kwa madhumuni ya ni kuinua na kustawisha hali ya maisha ya wanachama ambao ni waumini wa ushirika wa Kinondoni.  Upendo SACCOS ni muungano wa watu ambao wamekubaliana kuweka fedha zao pamoja na kukopeshana kwa len­go la kujiendeleza kiuchumi na kijamii na hatimaye kanisa kwa ujumla.

Shughuli kuu ya SACCOS hii ni kupokea Hisa, Akiba, Amana pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wanachama wake. SACCOS hii imeweza kufikia malengo yake kwa kutoa Elimu na Mafunzo kwa wanachama na wasio wanachama mara kwa mara.