Idara Ndani ya Ushirika wa Kinondoni

Image

Idara ya Kwaya Kuu

Idara ya Kwaya katika ushirika wa Kinondoni inajumuisha wakristo wenye vipawa mbali mbali vya uimbaji. Kusudi la Umoja wa Kwaya ni kumtukuza Mungu na kueneza injili kwa njia ya kuimba kwa Umoja. Idara ya kwaya huwajibika kufundisha nyimbo mpya, kufundisha elimu ya muziki ya kwaya, na kuandaa na kupanga kwaya kwa matukio maalum katika ushirika.

Mwalimu  wa Kwaya ndiye kiongozi wa Kwaya Kuu ya Ushirika. Kwa sasa ndugu Enea Kamwela ndiye Kiongozi wa Kwaya Kuu ya Ushirika. Baba Mchungaji Gentleman Mwansile, ni mlezi wa kwaya kuu ya ushirika.
Image

Idara ya Umoja wa Wanawake

Idara ya Umoja wa Wanawake katika ushirika wa Kinondoni inalenga  kuwaunganisha wanawake katika ushirika na kuwapa nafasi ya kutumia vipawa vyao kwa ajili ya maendeleo yao ya kiroho na kimwili wakimtumikia Mungu pamoja na kusaidiana wao kwa wao.

Lengo la idara hii ni kuhakikisha kuwa wanwake wanakuwa katika  maisha  ya  kumwabudu  Mungu katika Kristo Yesu ili kuendeleza ufalme wa Mungu kwa kuwaunganisha katika umoja wa rohoni pamoja na mpango wa sala. Pia kutumia  elimu  na  kazi  za  kujitoa  za  wanawake  katika kujenga na kuimarisha

Image

Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikristo

Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikristo katika ushirika wa Kinondoni ina jukumu la kuwasaidia  Vijana  ili  wampokee  Yesu  Kristo  kuwa  Bwana  na Mwokozi wao, kuwasaidia Vijana waishi kwa kufuata wito huo, wakishuhudia, wakitangaza habari njema, kuwasaidia vijana kujua namna ya kujitoa kutumika katika kazi mbalimbali za Kanisa na Taifa pamoja na kustawisha mizizi ya maisha ya Kiroho kwa njia ya Ibada ya pamoja kwa kujifunza Biblia na Sala. Pia kuendeleza umoja kati ya vijana katika   la Moravian pamoja na kushirikia na vijana wa makanisa mengine ndani na nje ya nchi, 

Image

Idara ya Watoto na Shule ya Jumapili

Idara ya Watoto na Shule ya Jumapili, ni idara inayolenga katika kuwalea watoto katika njia ya kumjua Bwana wetu Yesu Kristo toka utoto wao, na kuwatayarisha kuingia katika mafundisho ya Kipa Imara. Kwa sasa idara hii inaongozwa na Ndugu Donald Mwakatobe ambaye ndiye Mwalimu Kiongozi wa Idara ya Watoto na Shule ya Jumapili, akisaidiwa na walimu wenzake.

Kanisa limeweka shabaha ya Idara ya watoto na Shule ya Jumapili kuwa ni kama  ifuatavyo:

Image

Idara ya Uinjilisti na Misheni

Shabaha za kuanzishwa Idara ya Uinjilisti na Misheni ni pamoja na kueneza Injili na kuwaleta watu kwa Yesu ili wampokee kuwa Bwana wa Maisha yao, pamoja na kuimarisha mafundisho ya Kiroho katika ushirika.  Idara hii inaongozwa na Bi. Martha Shitindi  ambaye ndiye Katibu wa Idara ya Uinjilisti na Misheni wa Ushirika. Pamoja na mambo mengine idara hii inakazi ya kuandaa Mikutano ya Injili na Semina katika Ushirika. Idara hii inajukumu la kufindisha neno la Mungu ambapo kila Ijumaa jioni wakristo wa ushirika wa Kinondoni hukutana kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu na kushuhudia mambo makuu ambayo Mungu ameyataenda kwa waumini.

Image

Idara ya Ustawi wa Jamii

Lengo la kuwa na Idara ya Ustawi wa Jamii katika ushirika ni kuanzisha na kuendeleza huduma za msingi za kijamii kwa wahitaji walio ndani na nje ya Kanisa yaani jamii inayotuzunguka. Idara hii ina kazi ya kuhamasisha wakristo na jamii kwa ujumla juu ya wajibu wao wa kuwatafuta, kuwatambua na kuwahudumia watoto yatima, wazee, wajane, wagane na watoto waishio katika mazingira magumu/hatarishi, ili kuwapa huduma na malezi ya kikristo, kiroho, kimwili na kiakili ili  hatimaye wawe na matumaini ya maisha. Idara ina jukumu la kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuboresha Huduma za Jamii katika ushirika, 

Image

Idara ya Uwakili

Idara ya Uwakili ni moja katiya idara nane zinazounda ushirika wa Kinondoni. Uwakili ni mtu kuchukua jukumu la kuangalia mali ya mtu mwingine,kimsingi uwakili unaelezea au kuwakilisha utii kuhusu kutawala na kutiisha kila tunachokabidhiwa na Mungu. Dada Tonangile Mkisi ndiye kiongozi wa Idara ya Uwakili katika ushirika wa Kinondoni.

Kutimiza Wajibu
Ingawa Mungu ametukabidhi uumbaji wake tufurahie lakini vyote si vyetu bali ni vyake wajibu ni kuvitunza lakini mara nyingi tumelalamika kuhusu haki zetu,