Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe jumapili hii ameshiriki ibada pamoja na waumini wa kanisa la moravian Ushirika wa Kinondoni ikiwa ni pamoja na kutoa salamu zake za Mwaka Mpya.

Dk Mwakyembe amesema mwaka huu wizara yake itaendesha kampeni kubwa ya kitaifa ya Uzalendo na kuulinda utamaduni wetu, hivyo aliwasihi wanakinondoni kuwa mstari wa mbele katika kuwa wazalendo wa kulinda rasilimali za Taifa la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuheshimu mila na desturi za mtanzania.

Amesema wazazi wengi wamekosa muda wa kukaa na familia zao matokeo yake, wafanyakazi ama wadaidizi wa ndani hujikuta wakitumia muda mwingi kukaa na watoto, ikiwa ni pamoja na kutumia muda mwingi kujifunza tamaduni za nje kwa kutumia mitandao ya kijamii.