Idara ya Kwaya Kuu

Image
Idara ya Kwaya katika ushirika wa Kinondoni inajumuisha wakristo wenye vipawa mbali mbali vya uimbaji. Kusudi la Umoja wa Kwaya ni kumtukuza Mungu na kueneza injili kwa njia ya kuimba kwa Umoja. Idara ya kwaya huwajibika kufundisha nyimbo mpya, kufundisha elimu ya muziki ya kwaya, na kuandaa na kupanga kwaya kwa matukio maalum katika ushirika.

Mwalimu  wa Kwaya ndiye kiongozi wa Kwaya Kuu ya Ushirika. Kwa sasa ndugu Enea Kamwela ndiye Kiongozi wa Kwaya Kuu ya Ushirika. Baba Mchungaji Gentleman Mwansile, ni mlezi wa kwaya kuu ya ushirika.
Mwalimu wa Kwaya akisaidia na walimu wenzake, huongoza nyimbo katika ibada za ushirika pamoja na kuimarisha mafundisho ya Kwaya katika Ushirika. Pia kwaya kuu hushiriki kwenye makongamano/mikutano  pamoja na kwaya zingine za kanisa la Moravian kwa lengo la kufundishana/kupeana nyimbo.