Idara ya Ustawi wa Jamii

Image
Lengo la kuwa na Idara ya Ustawi wa Jamii katika ushirika ni kuanzisha na kuendeleza huduma za msingi za kijamii kwa wahitaji walio ndani na nje ya Kanisa yaani jamii inayotuzunguka. Idara hii ina kazi ya kuhamasisha wakristo na jamii kwa ujumla juu ya wajibu wao wa kuwatafuta, kuwatambua na kuwahudumia watoto yatima, wazee, wajane, wagane na watoto waishio katika mazingira magumu/hatarishi, ili kuwapa huduma na malezi ya kikristo, kiroho, kimwili na kiakili ili  hatimaye wawe na matumaini ya maisha. 

Idara ina jukumu la kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuboresha Huduma za Jamii katika ushirika, kuandaa  na  kutoa  Mafunzo  ya  Ujasiliamali  kwa  Watoto yatima, Wajane, Wagane na Watoto waishiyo katika Mazingira magumu/hatarishi ili waweze kujitegemea na kuwatafuta na kuwatambua Watoto yatima, Wajane, Wagane na Watoto waishio katika mazingira  magumu/hatarishi katika Ushirika.

Pia  idara  ina jukumu la kutafuta na kuushauri Ushirika njia mbalimbali za jinsi ya kuwasaidia na kuwatunza Watoto yatima, Wajane, Wagane na Watoto waishiyo katika Mazingira hatarishi, kusimamia   huduma   malimbali   zitolewazo   kwa   yatima, Wajane, Wagane,  na   Watoto   waishiyo  katika  Mazingira hatarishi, Wagonjwa wa muda mrefu katika Ushirika pamoja na kuratibu michango na misaada  yote  inayotolewa na wahisani au wafadhili toka ndani au nje ya nchi, ushirika au na muumini moja mmoja, pamoja na    kutunza  kumbukumbu za misaada iliyotolewa na wanufaika wa misaada hiyo.

Mama Kayanda…………. Ndiye Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Ushirika wa Kinondoni, na ndiye Mtendaji Mkuu wa Idara.