Idara ya Uinjilisti na Misheni

Image
Shabaha za kuanzishwa Idara ya Uinjilisti na Misheni ni pamoja na kueneza Injili na kuwaleta watu kwa Yesu ili wampokee kuwa Bwana wa Maisha yao, pamoja na kuimarisha mafundisho ya Kiroho katika ushirika.  Idara hii inaongozwa na Bi. Martha Shitindi  ambaye ndiye Katibu wa Idara ya Uinjilisti na Misheni wa Ushirika.

Pamoja na mambo mengine idara hii inakazi ya kuandaa Mikutano ya Injili na Semina katika Ushirika. Idara hii inajukumu la kufindisha neno la Mungu ambapo kila Ijumaa jioni wakristo wa ushirika wa Kinondoni hukutana kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu na kushuhudia mambo makuu ambayo Mungu ameyataenda kwa waumini.

 

Katibu wa Idara ya Uinjilisti na Misheni wa Ushirika ataongoza na kufundisha  mambo yayaohusu idara yake pamoja na kuandaa semina na mafundisho katika ushirika, pamoja na kufanya uinjilisti kwa wasio wakristo na waliojitenga na kanisa. Katibu wa Idara atafanya kazi zake akisaidiwa na kamati ya ushirika ya uinjilisti na misheni.  Mchungaji wa Ushirika Gentleman Mwansile ndiye Mlezi wa Idara hii.