Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikristo

Image
Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikristo katika ushirika wa Kinondoni ina jukumu la kuwasaidia  Vijana  ili  wampokee  Yesu  Kristo  kuwa  Bwana  na Mwokozi wao, kuwasaidia Vijana waishi kwa kufuata wito huo, wakishuhudia, wakitangaza habari njema, kuwasaidia vijana kujua namna ya kujitoa kutumika katika kazi mbalimbali za Kanisa na Taifa pamoja na kustawisha mizizi ya maisha ya Kiroho kwa njia ya Ibada ya pamoja kwa kujifunza Biblia na Sala. Pia kuendeleza umoja kati ya vijana katika   la Moravian pamoja na kushirikia na vijana wa makanisa mengine ndani na nje ya nchi, kuwahimiza vijana kujifunza ujasiriamali, stadi za kazi, uimbaji na muziki, kushiriki katika michezo na maigizo.

Idara hii pia ina lengo la kustawisha Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikristo katika Kanisa la Moravian na kushirikiana na vijana wa Makanisa mengine nchini na ulimwenguni kote,
kuwatia moyo vijana kufikiria juu ya wito wao, kutoa mafundisho juu ya uongozi wa Kikristo na kukuza Maendeleo ya Jamii na Maisha yao kwa ujumla, uwasaidia  vijana  kukuza  na  kuendeleza  sanaa  na  muziki,  na michezo  inayolenga  kutangaza  neno  la  Mungu  kwa  njia  ya  uimbaji  bora, maigizo, ngonjera, mashairi, Vichekesho, mipira na kazi za mikono pamoja na kudumisha mazingira endelevu ya kujiajiri na kuajiriwa.

Sifa za kujiunga katika umoja wa vijana zipo wazi kwa kijana wa kiume/kike mwenye umri kuanzia miaka 13 hadi 35. Katika ushirika wa Kinondoni, kuna makundi mawili ya vijana yaani vijana A na Vija B. Vijana wenye umri kuanzia miaka 13 hadi 17 huwa wapo katika kundi A. Katika Ushirika wa Kinondoni kundi hili linaitwa New Hope Kwaya. Vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 hawa wanaunda kundi B, ambapo katika uhsirika wa Kinondoni hujulikana kama Hekima Kwaya. Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya kikiristo ni jumuisho la makundi yote mawili ndani ya ushirika wa Kinondoni.

Kijana asiye mkristo aweza kujiunga umoja wa vijana akitazamiwa kwa muda wa Miezi sita; iwapo ataonyesha utii kwa umoja  na kwa kanisa atakuwa mwana Umoja wa kudumu, kama hataonyesha heshima na utii ataondolewa. Kijana anaweza kuondolewa kwenye umoja wa vijana akionekana kukosa sifa na kwenda kinyume na kanuni za idara.

Kijana yeyote anapokelewa katika Umoja wa Vijana bila kujali Taifa, rangi na kazi yake inayotambulika na kanisa. Vijana wa madhehebu mengine yanayotambuliwa na kanisa la Moravian  wanaweza  kuwa  washiriki  wa  umoja  huu  wakionyesha  cheti  cha utambulisho cha safari, Idara, na Ushirika husika.
 
Ngugu Makeke Mbwile ndiye Mwenyekiti wa Idara ya Umoja wa Vijana na Elimu ya Kikiristo wa Ushirika.  Kiongozi wa Vijana wa Ushirika anafanya kazi zake akisaidiwa na Kamati ya Vijana. Mwenyekiti wa idara pamoja na kamati yake ya uongozi, wanawajibu wa  kuwasaidia vijana wajitegemee kiuchumi, kutafuta njia za kueneza Neno la Mungu, kutembelea vijana, kuangalia  nidhamu,  utii  na  heshima  kwa kila mwana umoja. Vikundi hivi viwili yaani A na B huimba katika ibada pamoja na matukio mengine ya kikanisa kama vile sherehe na misiba.