Idara ya Umoja wa Wanawake

Image

Idara ya Umoja wa Wanawake katika ushirika wa Kinondoni inalenga  kuwaunganisha wanawake katika ushirika, na kuwapa nafasi ya kutumia vipawa vyao kwa ajili ya maendeleo yao ya kiroho na kimwili wakimtumikia Mungu pamoja na kusaidiana kama wana umoja. Idara hii inaongozwa na Mama Sara Mbonile.

Lengo la idara hii ni kuhakikisha kuwa wanwake wanakuwa katika  maisha  ya  kumwabudu  Mungu katika Kristo Yesu, pia kutumia  elimu  na  kazi  za  kujitoa  za  wanawake  katika kujenga na kuimarisha unyumba wa Kikristo, umoja na majirani, umoja wa ndugu katika Kanisa, pamoja na kushirikiana na wanawake wa Kanisa la Moravian mahali popote.

Idara hii inaundwa na kila mwanamke Mkristo mshiriki bila kujali kabila, rangi au taifa. Mwanamke mkristo aliyejitenga, hatakuwa na haki ya kupiga kura

wala kushika nafasi ya uongozi. Mwanamke  aliyewahi  kuwa  katika  umoja  huo  ushirika mwingine wowote, atawasilisha cheti cha utambulisho kutoka mahali alilikotoka. Wanawake   wa   makanisa   mengine   yanayotambuliwa   na Kanisa la  Moravian  waweza  kujiunga  iwapo  watakubali masharti ya idara hii.

Kila mwana wanawake wa ushirika wa Kinondoni huhudhuria  ibada  na mafundisho       mbalimbali ambayo huandaliwa na kanisa, pamoja na kuwasaidia watu wenye shida, kama vile waonjwa, yatima, wajane na wazee.

Pamoja na mambo mengine wanawake wa ushirika wa Kinondoni katika vipindi vyao hujifunza Biblia, nyimbo, hushauri juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Kanisa,  hufundisha ujasiriamali, hufundisha kushona, utunzaji wa nyumba zao na kanisa, hufundisha wanawake namna ya kuomba, ujasiri, uvumilivu, na kukwepa na kukabiliana na mifumo kandamizi na utandawazi kwa njia ya maombi.